Monday, September 3, 2007

TANZANIA YAOMBWA KUZINGATIA USHAULI WA MAREKANI

Chama cha Wananchi (CUF) kimeiomba serikali kuzingatia ushauri alioutoa Balozi wa Marekani Nchini, Bw. Michael Retzer, katika hafla ya kuwaaga watanzania, ambapo alitaka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) iwe taasisi huru itakayoweza kuchunguza rushwa mahali popote inapojitokeza. Taarifa iliyotolewa na Chama hicho jana ilisema kuwa balozi huyo alisema mpaka sasa TAKUKURU na Mkurugenzi wa Mashitaka wameweza kukamata `Samaki wadogo wadogo` wachache, lakini, akapendekeza kwamba samaki wakubwa si wachache na labda kuna hata `papa` kwenye dibwi hili la rushwa. Aidha, taarifa hiyo ilimnukuu balozi huyo akihimiza serikali kuacha kutumia mawakala inapofanya manunuzi makubwa ya serikali kwa sababu hatua hiyo inakaribisha rushwa. Kuhusu mwafaka wa CCM na CUF, Balozi huyo aliwasihi viongozi wa vyama hivyo kufanya kila juhudi kufikia makubaliano ya haki, yatakayo ridhiwa na pande zote mbili ili yaweze kutekelezwa kwa haraka kwa manufaa ya Wazanzibari na Watanzania kwa jumla.
CUF ? Chama cha Wananchi, tunaamini ya kuwa Serikali yetu itaupokea ushauri huo wa Balozi wa Marekani na kuufanyia kazi,` ilisema taarifa hiyo na kuongeza: `Hatuna budi kuzingatia kuwa Balozi Retzer alikuwa akiishi hapa hapa nchini kama balozi na kufanya kazi na serikali ya Tanzania kwa kipindi chote alichokuwepo.`
SOURCE: Nipashe

1 comment:

Anonymous said...

HERE WE GO AGAIN CORRUPTION CORRUPTION. THIS IS THE FIGHT WE MUST WIN FOR THE COUNTRY TO ACHIEVE RAPID DEVELOPMENT CHANGES THAT CAN BE SEEN BY A NORMAL TANZANIAN LIKE ME.