Wednesday, November 7, 2007

MAREKANI KUIPATIA TANZANIA DOLA MILION 645

2007-11-07 14:14:37 Na ITV Habari
Marekani itaipatia Tanzania dola milioni 645 kwa ajili ya kuendeleza sekta za usafirishaji, nishati na maji katika mikoa mbali mbali nchini ili kuondoa umaskini. Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam viongozi wa shirika la Millenium Challenge, tawi la Tanzania litakalotoa fedha hizo, wamesema kwa upande wa sekta ya usafirishaji, jumla ya dola milioni 373 zitatumika kukarabati barabara huko Zanzibar na Tanga na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha wilaya ya Mafia mkoani Pwani.
SOURCE: ITV

No comments: