Shahili lifuatalo hapo chini liliimbwa pamoja na ngoma za kitamaduni zilitumbuizwa na wana SERA . Kama kawaida wana SERA waliendelea kulitangaza taifa lao jinsi lilivyo na vivutio vingi kwa watalii.Pia waliweza kuwafaamisha watu wote waliofika katika sherehe hizo jinsi Tanzania ilivyo nchi ya Amani na jinsi gani imekuwa ikisaidia nchi jirani katika maswala mabali mabali likiwemo lile la kusaidia sana katika kuifadhi wakimbizi.Mungu ibariki Tanazania
Mtunzi na mwandishi wa shahili hili ni mTanzania mwenzetu
Ndugu Freddy Mwisomba.
1) Tunaanza na salamu, Kwa wote mliofika,
Tunachukua jukumu, Kuwapa habari njema,
Sisi tuliopo huku, Ni wana wa Tanzania.
Nchi yetu Tanzania,Twawakaribisha wote.
2) Nchi yetu Tanzania,Ni nchi yenye Amani
Watu wake wakulima, Pia na wafanyakazi
Watoto wana furaha, Tamaduni zake safi.
Nchi yetu Tanzania, Twawakaribisha wote.
3) Watu wote mliopo, Mnaujua mlima,
Mlima Kilimanjaro, Upo kwetu Tanzania
Wasimama kama nguzo, Imara ya Africa.
Nchi yetu Tanzania,Twawakaribisha wote.
4) Ziwa kubwa Africa, Ni ziwa Victoria
Lipo kwetu Tanzania, Kenya pia na Uganda
Ni kivutio kikubwa, Wote mje kukiona
Nchi yetu Tanzania, Twawakaribisha wote.
5) Mbuga zetu za wanyama, Zapendwa na watalii,
Mikumi pia Manyara, Simba, Faru watawala,
Wapatikana Wanyama, Adimu kwenye dunia,
Nchi yetu Tanzania, Twawakaribisha wote.
6) Mira za Watanzania, Zimejengwa kwa busara,
Mdundiko Bongo fleva, Ngoma zetu tunacheza
Mbalimbali makabila, Kiswahili twazungumza
Nchi yetu Tanzania, Twawakaribisha wote.
7) Twapendana na wenzetu, Wakenya na Waganda
Biashara kwenda juu, Maendeleo makubwa,
Ushirikiano huu, Unaendelea sana,
Nchi yetu Tanzania, Twawakaribisha wote
8) Si kama Tunajigamba, Ila Twasema ukweli
Mungu ametujalia,Nchi yetu ya Amani,
Aridhi yenye rutuba, Mazao yanashamiri
Nchi yetu Tanzania, Twawakaribisha wote.
9) Matatizo pia yapo, Kama vile maleria,
Gonjwa latupiga kumbo, Twahitaji kuliua,
Tutaja liweka kambo, Wote mkisaidia,
Nchi yetu Tanzania, Twawakaribisha wote.
10) Mwisho Twawakaribisha, Wawekezaji Nchini
Watalii mje ona, Nchi yetu hii nzuri,
Wote mliofika hapa, Muijue nchi hii,
Nchi yetu Tanzania, Twawakaribisha wote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment